Ni
kile kinachoitwa Chama Cha Mpira tawi la mipango kuvaa joho la serikali ya
wanafunzi chuoni hapa. Chama Cha Mpira tawi la chuo cha mipango na maendeleo vijijini
Dodoma kimegeuka taasisi yenye kuamua maswala yahusuyo wanafunzi chuoni hapa
kinyume na taratibu. Tumeshuhudia matukio mengi ya kushangaza na yenye kuzua
sintofaham nyingi. Tumekuwa tukijiuliza kwama kweli serikali ya wanafunzi
chuoni hapa kama kweli ipo? na kama kweli ipo je niyawanachuo au ni ya Chama Cha Mpira??
Serikali
ya wanafunzi chuoni hapa imegeuka kuwa kibaraka wa Chama Cha Mpira hadi kufikia
hatua mawaziri wa serikali ya wanafunzi kukatwa posho zao kwaajili ya kulipia
kodi ya ofisi ya chama hicho chuoni hapa
Kuelekea
mchakato wa uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapa, yameanza kusikika
mengi yenye sura ya hujuma na rushwa ndani na nje ya serikali ya wanafunzi
chuoni hapa na hasa ndani ya Chama Cha Mpira.
Sintosita kuyaweka wazi machache hasa yale
yanayohusiana moja kwa moja na mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi wa tano.
Tume ya uchaguzi.
Kama
ilivyo kawaida tume ya uchaguzi hupatikana kwa kila darasa kutoa watumbe
wawilia ambao hupitishwa kwa kupigiwa kura madarasani mwao na baadae kufanyiwa
mchujo na bunge ili kupata idadi ya wajumbe 14 watakao unda tume ya uchaguzi.
Kwa
tarifa kutoka chanzo kinachoaminika ni kuwa kwa mwaka huu Chama Cha Mpira tawi
la mipango kiliandaa mkakati wa kumshinikiza raisi wa serikali ya wanafunzi kuteua wabunge wengine wasio
pungua hamsini (50) ili kufanya mabadiliko ya katiba na kumpa raisi mamlaka ya
kuteua tume ili waweze kupitisha makada wa chama hicho kuwa wajumbe watume kwa
lengo la kuwapitisha wagombea walio chaguo la viongozi wa chama. Mpango huo
uliposhindikana Chama Cha Mpira kimeamua kurudia njia yao ya zamani ya
kuzunguka madarasani kuandaa makada watakao gombea ujumbe wa tume ya uchaguzi
kwa lengo la kuwapitisha makada kugombea nafasi ya uraisi.
Katika
kuhakikisha mkakati huo dhalimu unafanikiwa Chama Cha Mpira chuoni hapa kilipanga
kinamuandaa aliyekuwa raisi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapa kuwa
mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kitu ambacho kimeshindikana baada ya wapenzi wa
haki chuoni hapa kuanza kupiga kelele kuhusiana na swala hilo.
Chama
Cha Mpira kimevuka mipaka hadi kufikia hatua ya kuwafanyia mchujo watia nia wa
ngazi ya uraisi, Mchujo huo wa aina yake uliongozwa na viongozi wa Chama Cha
Mpira ngazi ya wilaya.
Rushwa.
Ndani
ya Chama Cha Mpira tawi la mipango rushwa sio jambo la kificho tena. Sasa ni
dhahiri kuwa Chama Cha Mpira mipango kinanuka rushwa. Kutokana na hofu ya watia
nia wa ngazi ya uraisi kuwa kubwa, Chama Cha Mpira tawi la mipango kimeandaa
mkakati unao ongozwa na katibu wa chama hicho
wa kuwashinikiza watia nia wote kutoa rushwa ya kiasi cha Tsh, laki tano
(500,000) ili kupata kile kinachoitwa Baraka za chama ili waweze kupata nafasi
ya kugombea.
Ila
ikumbukwe kuwa, huu ni mwendelezo wa mchakato wa kuhakikisha wagombea walio
chaguo la chama hicho wanashinda. Lengo kuu la mkakati huo ni kuwanyima haki
wanafunzi wenye itikadi ya chama hicho kugombea ili wale mgombea walio chaguo
la viongozi wa chama waweze kupenya.
Jambo
hili ni rushwa na nijambo la kupingwa ndani na nje ya chama hicho kwa ustawi wa
jamii ya wanafunzi chuo hapa na taifa kwa ujumla.
Hadi
sasa yapo makundi yasiyopungua nane yanayojinasibu kushinda kiti hicho cho cha
uraisi chuoni hapa.
Team;
Nyeupe nyeupe, Nyeusi nyeusi
Team;
Kweka (waziri wa afya wa MISO 2017/2018)
Team;
Azizi (waziri wa fedha MISO 2017/2018)
Team;
Mtatiro
Team;
Eliudi
Team;
Musa Lameck (mrashia)
Team;
Kanali
Team;
Wambura
Siku
za usoni tutegemee video na sauti za baadhi ya wagombea na hasa mipango michafu
ya Chama Cha Mpira kuelekea uchaguzi huu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapa.
By
Mipango Media
Comments