MISO STUDENTS BARAZA Katiba ya MISO inatambua uwepo wa student baraza kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 12 ya katiba MISO. Ibara ya 12(1) inaeleza kuhusu uwepo au uanzishwaji wa student baraza kwenye kila tawi la chuo cha mipango. Ibara hii ya 12 ina ibara ndogo ndogo tisa zenye vipengele mbali mbali vinavyotoa utaratibu wa jinsi student baraza linavyopaswa kufanyika kwenye kila tawi la chuo cha mipango. Katika makala hii ya leo nitaangazia ibara ndogo ya 3(a na b) ya ibara hii ya 12, ambayo inahusu aina na idadi ya mikutano ya student baraza. Ibara ndogo ya 3(a) inaeleza kuwepo kwa mikutano miwili ya kawaida(ordinary meeting)ya student baraza ambayo tarehe za mikutano hiyo hutolewa mapema na serikali ya wanafuzi. Pia ibara ndogo ya 3(b) inazungumzia kuwepo kwa mikutano ya student baraza ya dharura (extra ordinary meeting) pia imetoa utaratibu wa jinsi mikutano hiyo ya dharura itakavyoitishwa. Imekuwa ni mazoea kwa serikali kutotimiza sheria hii kwa wana MISO wa
Comments