Kutokana na kutokujitambua na
kukubali kutawaliwa na hisia za miili yetu. Tumeishi kuitumikia miili yetu
kwenye maswala ya ngono badala ya miili yetu kututumikia sisi kwenye maswala ya
upendo, ndio maana mataifa ya magharibi (kupitia sera zao za mambo ya nje)
yameweza kutupangia hata ustaarabu wa tendo la ndoa na maswala mazima ya uzao. Matumizi
ya vithibiti mimba (njia za kisasa za uzazi wa mpango) ni moja wapo tu ya nja zinazotumiwa
na mataifa ya magharibi za kuthibiti ongezeko la idadi ya watu duniani na hasa
mataifa ya dunia ya tatu. Madhara ya njia hizi ni mengi yanayojulikana ila wamezidi
kutusisitiza kutumia. Nasi pasipo kujali ama kufanya tafiti za kutosha,
tumekuwa wepesi kuzitumia kwasababu tu zinarahisisha ufanywaji wa tendo la ndoa
wakati wowote na kwa mtu yeyote.
“Despite what the world teaches,
nobody has died from not having sex. Rather millions have died from having too
much sex. (by Brian Clowes )
Napata ujasiri kusema wanaotumia
njia hizi ni wauwaji wa watoto wao wenyewe kwani njia hizi zina madhara mengi
sana na baadhi hutoa mimba changa (they allow fertilization but hinder
implantation) Ni wito wangu kwa jamii hii ya wasomi tusimame kulinda afya zetu
na za watoto wetu yaani kizazi kijacho cha taifa letu.
Remember that each human life born or unborn,
is sacred, unique and precious in the eyes of God, So don’t do anything to harm
another person or pressure or support anyone in killing of unborn child
By
Gabriel Saudari
Monday, 28 May 2018
Comments