MISO STUDENTS BARAZA
Katiba
ya MISO inatambua uwepo wa student baraza kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya
12 ya katiba MISO.
Ibara
ya 12(1) inaeleza kuhusu uwepo au uanzishwaji wa student baraza kwenye kila
tawi la chuo cha mipango.
Ibara
hii ya 12 ina ibara ndogo ndogo tisa zenye vipengele mbali mbali vinavyotoa
utaratibu wa jinsi student baraza linavyopaswa kufanyika kwenye kila tawi la
chuo cha mipango.
Katika
makala hii ya leo nitaangazia ibara ndogo ya 3(a na b) ya ibara hii ya 12,
ambayo inahusu aina na idadi ya mikutano ya student baraza.
Ibara
ndogo ya 3(a) inaeleza kuwepo kwa mikutano miwili ya kawaida(ordinary
meeting)ya student baraza ambayo tarehe za mikutano hiyo hutolewa mapema na
serikali ya wanafuzi. Pia ibara ndogo ya 3(b) inazungumzia kuwepo kwa mikutano
ya student baraza ya dharura (extra ordinary meeting) pia imetoa utaratibu wa
jinsi mikutano hiyo ya dharura itakavyoitishwa.
Imekuwa
ni mazoea kwa serikali kutotimiza sheria hii kwa wana MISO wakidai kuwa sheria
hii inatoa mwanya kwa serikali kuitisha mikutano hii pale tuu inapohitajika.
Naomba nitumie nafasi hii kwanza kuweka sawa kuhusu upotoshaji huo mkubwa,
kwani ni uongo mkubwa unaolenga kufifisha ama kuzima kabisa sauti ya wanamiso
kwenye mambo yanayowahusu hasa utendaji kazi wa serikali iliyoko madarakani. Tafsiri ya sheria imekuwa ikifanywa kwa
kulinda maslai ya serikali.
Mfano,
vikao vya kawaida vya bunge vinatajwa na katiba hi kwenye ibara ya 13(1) kwa
lugha ile ile inayotaja kuwepo kwa student baraza “There shall be an Institute
Students Representatives Council (ISRC) at every Campus, The ISRC shall convene
two ordinary meetings in a semester”. Chakushangaza ni kuwa inatekelezwa tu ile
ya bunge tena kwa utaratibu ule ule uliotajwa bila kupindisha matakwa ya katiba
lakini sivyo inavyofanywa kwa Ibara ya 12(1)a inayotaja kuwepo kwa student
baraza.
Kwa
uzoefu wangu mdogo wa miaka mitano ndani ya chuo cha mipango. Kwa kumbukumbu
zangu, sijawahi kushuhudia mikutano ya kawaida ya student baraza (ordinary
meeting) kama inavyotajwa kwenye katiba ya MISO badala yake ni mikutano ya
dharura(extra ordinary meeting) inayopewa jina la mkutano wa kawaida kinyume na
utararibu.
Tabia
ya viongozi wengi au serikali nyingi dhaifu zimekuwa zikifanya mambo yake kwa
dharura hasa mambo yahusuyo mijadala ili kunyima fursa kwa wadau kujianda
vizuri kwaajili ya mjadala wa jambo fulani. Tabia hii tumeiona hata kwenye
serikali zilizopita. serikali nyingine hazikuthubutu kabisa hata tuu kutii
sheria hii na kuitisha student baraza. Serikali zilizojitahidi zilijaribu kuitisha
kwa dharura mikutano hiyo vivyo hivyo serikali hii chini ya raisi wetu Judith
Rajabu Mlanda imefwata nyayo na kutunyima wana MISO haki hii ya msingi ya kukaa
na kujadili mambo yanayotuhusu. Na hii ni kwasababu ya woga uliotanda ndani ya
serikali kutokana na mwenendo mbovu wa serikali hii kwani harufu ya Rushwa na
ubadhirifu wa rasilimali za MISO umeshaanza kusikika.
Kuna
umuhiu mkubwa sana wa kuwepo kwa student baraza kama inavyoelekezwa kwenye
katiba yetu. Umuhimu huu unatokana na nafasi kubwa ya maamuzi iliyopewa student
baraza. Ibara ya 12(2) ya katiba ya MISO inatambua student baraza kama ngazi ya
juu kabisa ya maamuzi ndani ya MISO (The Student Baraza at every Campus shall
be the supreme organ of the Organization at the particular Campus) kwa
kuitambua nafasi hii ya student baraza napata ujasiri mkubwa na bila kusita
kupaaza sauti kudai haki hii adimu kwa wanamiso wote.
Tumeshuhudia
baadhi ya mawaziri tunao wategemea kuwasaidia wana MISO wakiwa mstari wa mbele
kubeza na kumkejeli yeyote Yule anayejaribu kuhoji kuhusu mwenendo mbovu wa
serikali. Tabia hii imeonekana sana kwa waziri wa habari na burudani Ndg.
Mungia Ally Kiruasha ambaye amekuwa akifanya kazi ya kuwavunja moyo wale wote
wanaojaribu kujua nini hasa kinaendelea ndani ya serikali ya MISO.
Natoa
wito kwa wana MISO kuzidi kuwa na mshikamano na kutorudi nyuma, kwani hata kwa
kunyimwa haki hii ya kukaa na kujadili mambo yetu kwa lengo la kuficha uchafu
wa serikali hii, Tutazidi kupaaza sauti ndani na je ya MISO ila kama kuna namna
yoyote ya ubadhirifu wa rasilimali za MISO uweze kuwekwa wazi na wahusika
waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili.
Imesambazwa na UHURU WA MAWAZO IRDP.
Comments