Ni kile kinachoitwa Chama Cha Mpira tawi la mipango kuvaa joho la serikali ya wanafunzi chuoni hapa. Chama Cha Mpira tawi la chuo cha mipango na maendeleo vijijini Dodoma kimegeuka taasisi yenye kuamua maswala yahusuyo wanafunzi chuoni hapa kinyume na taratibu. Tumeshuhudia matukio mengi ya kushangaza na yenye kuzua sintofaham nyingi. Tumekuwa tukijiuliza kwama kweli serikali ya wanafunzi chuoni hapa kama kweli ipo? na kama kweli ipo je niyawanachuo au ni ya Chama Cha Mpira?? Serikali ya wanafunzi chuoni hapa imegeuka kuwa kibaraka wa Chama Cha Mpira hadi kufikia hatua mawaziri wa serikali ya wanafunzi kukatwa posho zao kwaajili ya kulipia kodi ya ofisi ya chama hicho chuoni hapa Kuelekea mchakato wa uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapa, yameanza kusikika mengi yenye sura ya hujuma na rushwa ndani na nje ya serikali ya wanafunzi chuoni hapa na hasa ndani ya Chama Cha Mpira. Sintosita kuyaweka wazi machache hasa yale yanayohusiana moja kwa moja na mchakato wa uchag